Jump to content

Tarekh ya mitume:Ibrahim

From Wikisource

Tarekh ya mitume:Ibrahim Mtume wa Tawhidi Ibrahim (‘Alahyi Salaam) Mtume wa Tawhidi, hilo linadhihiri katika Historia yake; hivyo ndio maana Allah akamsifu kwa kusema: “Hakika Ibrahim alikuwa mfano mwema, mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.” (16:120);

Ibrahim aliishi pamoja na kaumu ya washirikina, bali baba yake alikuwa mmoja wa wanaoabudu masanamu na mmoja miongoni mwa wanaoyatengeneza na kuyaabudu, Ibrahim akaanza kujadiliana na baba yake pamoja na kaumu yake: “Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake, Azar: Unayafanya masanamu kuwa ni miungu? Hakika mimi nakuona wewe na watu wako mmo katika opotofu ulio wazi.” (6:74)

Na akapinga yaliyokuwa kwa kaumu yake kwa hoja madhubuti ushirikina wao na akawa anaangalia katika alama na dalili za kuwepo kwake Allah Ta’ala: “Na ulipo muingilia usiku akiona nyota, akasema: Huyu ni Mola Mlezi wangu. Ilipo tua akasema: Siwapendi wanao tua.” (6:76);

Yaani: kuzama kwa nyota: “akasema: Siwapendi wanao tua. Alipo uona mwezi unachomoza…” (6:76-77),

Yaani: Kuchomoza kutoka kwenye upeo wa macho, na akaona baadhi ya watu wakiyaabudu: “…alisema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu…” (6:77).

Akapinga matendo yao, huku akistaajabia ibada zao!! Aliitumia fursa hiyo: “…Ulipotua…” (6:77);

Yaani kupotea chini ya upeo wa macho, alielekea kwa watu wake na kuwaambia: “…akasema: Kama Mola Mlezi wangu hakuniongoa, nitakuwa katika kaumu walio potea. …Na alipo liona jua linachomoza” (6:77-78),

Na akawaona watu wakinyenyekea mbele yake: “…akasema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Huyu mkubwa kuliko wote….” (6:78)

Akapinga matendo yao!! Akashangazwa ni kwa nini wamefanya jua kuwa Mungu wao?! “…Lilipo tua…” (6:78),

Na kupotea machoni, aliwaelekea watu wale ambao walikuwa wakiiabudia, akawaambia: “…alisema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayo fanyia ushirikina. …Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu sawa sawa kwa aliye ziumba mbingu na ardhi, wala mimi si miongoni mwa washirikina.” (6:78-79).

viungo vya nje

[edit]

mtume musa

[1]