Swalah ya Janeza
Swalah ya Janeza
[edit]Miongoni mwa hukumu za Swalah ya jeneza 1. Mwenye kukosa Swala ya maiti atamswalia kaburini kabla ya kuzikwa au baada yake, kwa hadithi iliyothubutu kwa Mtume ﷺ katika kisa cha mwanamke aliyekuwa akisafisha msikiti alipo kufa na kuzikwa Mtume ﷺ alikwenda akamswalia kaburini [ Imepokewa na Bukhari.].
2. Inapendekezwa kutayarishiwa watu waliofiliwa chakula, kwa kuwa wao wameshughulishwa na msiba na kutotayarisha chakula.
Kwa ilivyopokewa kuwa jamii ya Jaafar walipofiliwa, Mtume ﷺ akasema: (Wafanyieni jamii ya Jaafar chakula, kwa kuwa wamejiwa na jambo la kuwashughulisha) [Imepokewa na Abuu Daud.].
Kuwafanyia chakula waliofiliwa
3. Kumlilia maiti, bila kujitia hasira wala kuinua sauti wala kuomboleza, kunafaa. Mtume ﷺ Amesema alipokufa mwanawe, Ibrahim: (Kwa hakika jicho linatokwa na machozi na moyo unasikitika, na hatusemi isipokuwa linalomridhisha Mola wetu. Na sisi, ewe Ibrahim!, tuna huzuni) [Imepokewa na Bukhari.].
4. Shahidi wa vitani atazikwa na nguo zake alizouawa nazo, na haoshwi wala haswaliwi, kwa haditi iliyothubutu kwamba Mtume ﷺ aliamrisha wazikwe mashahidi wa vita vya Uhud wazikwe wakiwa na damu zao na wasioshwe [Imepokewa na Bukhari.].
Shahidi huzikwa akiwa na nguo zake
5. Akifa aliye kwenye hali ya Ihramu ya Hija au ya Umra, ataoshwa na hatatiwa manukato, wala hatafinikwa kichwa chake na ataswaliwa.
Hii ni kwa iliyothubutu kwamba Mtume ﷺ alisema kuhusu mtu aliyekufa naye yuko kwenye Ihramu ya Hija: (Muosheni kwa maji na mkunazi, na mkafinini ndani ya nguo mbili, wala msimfinike kichwa chake, kwani yeye atafufuliwa Siku ya Kiyama katika hali ya kuleta Labeka) [Imepokewa na Bukhari.].