Jump to content

Swahili Tales/Utumbuizo wa Gungu

From Wikisource
297784Swahili TalesUtumbuizo wa Gungu1870Edward Steere

[ 474 ]

UTUMBUIZO WA GUKGU.
GUNGU LA KUFUNDA.


Pani kiti, nikae kitako,
Tumbuize waugu Mananazi,
Tumbuize wangu manamke,
Mpangua hamu ua simanzi.
Husimama tini wa mlango
Kiwa nde kwenda matembezi,
Chiwa nde kaingia sliugbuli,
Kiwaambia wakwe waandazi,
Kamwambia Sada na Kehema
Mwandani pasiwa ajizi,
Wandani, tendani haraka,
Mwaudae wali na mtuzi.
Akimbona nimelimatia,
Kaondoa chakwe kiyakazi,

[ 476 ]

Mwangalie usita wa yumbe,
Ao kwao kwa fumo wa ezi,
Mwangalie tengoni pa uduze,
Ao kwao kwa mama shangazi,
Kampate, hima uye naye.
Watendani hatta njeu shizi
Kamwambia, bwana, waamknwa,
Tenda hima, sifanye ajizi,
Yanga lako wimie tutule,
Na matoni hutuza tozi.
Kaamba tende tangulia, naja,
Kamtuze, ate simanzi,
Kamwandama nyuma kiongoya,
Akinuka meski na mbazi.
Akiingia kampa salamu,
Kamjibu mwana wa Hejazi.
Saa hiyo kaondoka akaima,
Kamwaudika mkono wa fuzi,
Kamwombea Muimgu Jabari,
Ewe mama, Mola ngwakujazi.

[ 478 ]

Akiinua mkonowe mwana
Kaupeeka juu la mwanzi.
Akaangua kisuto clia kaye,
Cha kinisi chema matorazi,
Ka'mweka kituzo cha mato,
Buni ami, mwana wa shangazi.
Kimwambia, bwana na tukae,
Siimemno, ukataajazi.
Nitiani hoyo Timi aye,
Na anguse, ate masindisi,
Apakue pilao ya Hindi,
Mzababu isiyo mtuzi.
Ete kiti chema cha Ulaya,
Na sinia ujema ya Shirazi
Munakaslii inakishiweyo,
Na sahani liuug'ara ja mwezi.
Kaamuru khodama na waja,
Ai nini hamtnmbiuzi ?
Bassi hapo akamwandikia
Naye Timi yushishiye kuzi,

[ 480 ]

Yapejeto maji ya zabibu
Kimiiyesha kama mua shizi.
Kimlisha akimrehebu
Kimwonya kwema maozi.
Kimlisha tambuu ya Siu,
Ya layini layini ya Ozi,
Kiukuta kuno kimwakiza,
Kwa iliki pamwe nn jozi.
Nikumele kusifu mbeja
Mteule wangu Mananazi.

GUNGU LA KUKWAA.

Mama, nipeeke, haoe kaoe
Urembo na shani Ungama,
Haoe mnara mpambe mpambe,
Uzainyeo heshima.
Na wenyi kupamba patoto patoto.
Wavete vitiudi na kama,

[ 482 ]

Wavete saufo ziemba ziemba,
Na mikili bee na uyuma.
Wavete libasi teule teule,
Kwa zitnana bee na nyuma.
Watukuze panga iigao ua ugao.
Mtu hutosliea kuona.
Kujile Mugazidja na kubu na kubu,
Ujile kutaka harubu.
Kujile Mgala na mata na mata,
Ujile kiitaka kuteta.
Tutawatilia iikuta iikuta,
Wasituiugilie myini.

[ 474 ]


[ 474 ]

The same in common Swahili.
 
Npeni kiti, nikae kitako,
Nipembeze Mananazi wangu,
Nipembeze mwauamke wangu,
Aniondoa bamu na simanzi.
Husimama chini ya mlango
Nikitoka kwenda kutembea,

[ 475 ]

Nikitoka kufanya shughuli,
Huwaambia watumishi wake,
Akamwambia Sada na Rehema
Pikeni msikawilie.
Pikeni, mfanya upesi,
Mpike wali na mchuzi.
Akiniona nimekawilia,
Humtuma kijakazi chake.

[ 476 ]

Mtezame njia ya Sultani,
Ao kwao wa mfahne aliyetawala,
Mtezame vikaoni vya nduguze,
Ao kwao kwa mamaye, shangazi Lake,
Kamshike, upesi uje naye,
Wafanya nini hatta wakati huu?
Kamwambia, Bwana, unakwitwa,
Twendo npesi, sifanye uvivu,
Kukawilia kwako huchoka kusimama
Na machoni yatoka machozi.

[ 477 ]

Kamwambia, twende tangulia nnakuja,
Kamtulize, awache majonzi,
Kamfuata nyuma kwa tambo,
Akinuka mesiki na ambari.
Akipita akamwamkia,
Kamjibu mtoto wa Hejazi.
Marra hiyo akaondoka akasimama.
Aka'mweka mkono wa bega,
Kamwombea Muungu Jabari,
Ewe mama, Muungu atakujalia.

[ 478 ]

Akainua mkono Mwana
Akaupeleka jmi ya mwanzi.
Akaangua kisuto cha kikale,
Kizuri kimetariziwa,
Akamweka kitulizo cha macho.
Mwana wa ndugu wa babaye, na mwana wa shangazi.
Akamwambia, Bwana tukae kitako,
Usisimame mno, ukafanye uvivu.
Mwiteni huyo Time aje,
Upesi, awache usingizi,

[ 479 ]

Apakue pilao ya kihindi,
Ya zabibu haina mchuzi.
Lete kiti kizuri cha Ulaya,
Na sinia njema ya Shirazi
Imetiwa nakishi,
Na sahani inang'ara kama mwezi.
Akanena watumwa na waje,
Kwa nini hamwimbi?
Marra hiyo akaandikiwa
Na Time ameshika guduwia,

[ 480 ]

Imetiwa maji ya zabibu
Akimoywesba kama muyua tembo.
Akimlisba akimrai
Akimwonyesba kwema malazi.
Akimlisba tambuu ya Siyu,
Laini laini ya Ozi,
Akaikunja akimtia kinwani,
Na iliki pamoja na lozi.
Nimekoma kusifu mwanamke
Wa kuchagua waugu Mananazi.

[ 481 ] The second figure in common Swahili.

Mama, nipeleke hatazame
Uzuri na pambo Ungama,
Hatazame mnara umepambwa,
Uliotengenezwa kwa heshima.
Tva waliopamba watoto,
Wamevaa timbi na vidani,

[ 482 ]

Wamevaa sarufu na vilemba,
Na tamvua mbele na nyuma.
Wamevaa nguo za kuchagua,
Kwa watumwa mbele na nyuma.
Wamechukua pauga na ngao.
Mtu hutaajabu akiona.

[ 483 ]

Amekuja Mngazidja na kopo,
Amekuja kutaka vita.
Amekuja Mgala na uta,
Amekuja kutaka kupigana.
Tutawajengea ukuta,
Wasituingilie mjini.