Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/96

From Wikisource
This page has been proofread.
76
SULTANI DARAI.

ninakwenda zangu, nije nikukute papa hapa. Paa akatoka mbio hatta jua lalipopata mafungulia ya ng'ombe makuu, ametokea ile nyumba ya Sultani. Marra asikari waliowekwa katika njia kumngojea Sultani Darai atakapokuja, alikwenda asikari mbio, akamwambia Sultani, Sultani Darai anakuja, nimemwona paa anakuja mbio.

Sultani akatoka na watu wake kwenda kumlaki kule katika njia. Alipokwenda hatta alipokoma nussu ya njia, wakakutana na paa. Paa akamwambia, Sabalkheiri, bwana. Akamwambia, marahaba paa, hujambo. Akamwambia, bwana, sasa si niulize neno, siwezi kuvuta hatua hapa na hapa.

Sultani akanena, gissi gani paa? Akamwambia, Nimekuja na Sultani Darai, na katika njiani, nimetoka mimi naye peke yetu, hakufuatana na mtu yo yote, zayidi yangu mimi. Tukaja hatta katika mwitu, tukakutana na haramia, wakamkamata bwana wangu, wakamfunga, akapigwa na haramia sana, wakamnyang'anya na vyombo vyake alivyokuwa navyo vyote, hatta kitambi cha kuvaa chini wamemvua. Bassi hapo alipo bwana kama siku aliozaliwa na mamaye.

Sultani akatoka mbio na waaskari, wakaenda mbio tena hatta nyumbani kwake. Akamwita mtunga frasi, akamwambia, Tandika frasi katika banda, alio mwema katika frasi wangu, na matandiko yale yalio mema ninaopandia mwenyewe. Akamwita mjakazi wake—Henzerani! Akamwitika, Labeka, bwana. Akamwambia, fungua kasha kubwa la njumu, toa bahasha moja ya nguo. Akaenda akifungua, akaleta bahasha ya nguo. Sultani akifungua, akatoa joho moja nyeusi ilio njema sana, akatoa