Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/66

From Wikisource
This page has been proofread.
46
SULTANI DARAI.

nguo, cha tatu hichi kilemba, la nne huu mkaja, la tano huu ubeleko, cha sita hichi kiosha miguu, cha saba hichi kifungua mwango, na hizi ndizo nalizopewa kukabithi, na kipa mkono amesema atakuja nacho mwenyewe, naye akasema yeye huko yu tayari akungoja wewe kwenda kumwita. Amwambia, nami sina shughuli, muhulla wangu leo, hatta kesho atapata mkewe.

Akachukua nguo zake, akaenda nazo ndani kwa mkewe. Akamwambia, mke wangu mwite mtoto kumwonya nguo zake, kumwonya na mahari yake, afanye atakalofanya.

Akamwita mtoto, Mama njoo, hizi nguo zako zimetoka kwa mchumba wako, na haya mahari yako, na hizo zalizobaki ni ada zetu, ni mimi na babayo.

Akamwambia, bassi mama, laliokwisha kwenu, mimi naweza kulirudi? Ni lile mpendalo nami nimependa, siwezi kumpaka baba angu uso mavi, apitapo asipate kufunua macho, napenda nimfurahishe baba yangu apitapo afunue macho, acheke kama ada, kama walimwengu wachekavyo, anene kama ada, walimwengu wanenavyo, atembee kama ada ya walimwengu, watembeavyo, nami sipendi kuipata kasarani ya baba yangu, napenda kama watu wakaavyo na baba zao, nami ni vivyohivyo.

Akamwambia, vema mwanangu, umenena maneno yapendezao, mimi nalithani mwanangu, utaniinamisha uso mbele za watu nawe umeniinua uso mbele za watu. Muungu akupe kukua mwanangu, uwe na moyo mzuri kama haya walionijibu, kwani ni maneno yenyi njia, nami baba yako nimefurahiwa.

Bassi, wakakaa kitako nyumbani wakati kutengeneza