Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/60

From Wikisource
This page has been proofread.
40
SULTANI DARAI.

chakula chema, umvike nguo njema, umtandikie kitanda chema, umzumgumze mazumgumzo mema, huyu ndiye mamayo, huyu ndiye babayo, huyu ndiye mumewo, huyu ndiye shogayo, huyu ndiye mwanao. Bassi, tafáthali mtunze sana mtoto.

Mwanamume akaondoka hatta akafika kwake mwanamke wake. Mkewe amepata habari, kama mumeo amenunua suria, ame'mweka nyumba marehemu mkewe, bassi akanena mwanamke, nyumba hilo akija haingii, atamrudia suria hiyo, aliko'mweka, ao tutakwenda zetu kwa Shekhi sasa hivi, akaniache, simtaki mume huyu tena. Ah! mume akinunua suria, miye anitakia nini tena?

Marra mwanamume amekuja, mwanamke akatwaa mguu moja huku, na moja huku, akatanua katika mwango, kungoja mumewe akija, asipate njia ya kuingia ndani, akatanua na yote mikono miwili mwangoni.

Alipotokea mumewe, amwambia, Rudi, rudi, koma sije nyumbani kwangu, usije, huko ulikonunua suria na nyumba ulio'mweka, rudi, kakae kuko huko, nyumba hii yone paa usije mwangoni kwangu.

Oh! Mwanamke, una wazimo uningoje kwanza ukaniuliza. Pa! ukanirukia. Niite faraghani nyumbani uniulize, umekaa mwangoni hapo mguu huku, mguu huku, mkono huku mkono huku, umewamba mwango, watu pia wakipita wakuone umesimama hivyo katika mwango, hutahayari nafsi yako?

Sitaki maneno yako leo, rudi kuko huko, rudi kuko huko, usiingie nyumbani mwangu.

Ee, bibi yangu, tafáthali uniache haneno nayo maneno matatu.