Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/54

From Wikisource
This page has been proofread.
34
SULTANI DARAI.

kwa kuwa mwanao, ao nimetukana mtu, bass umenifunga kunirudi ili situkane tena mtu, ao nimekwiba mali ya watu, umekuja kustakiwa, bassi umenifunga kunirudi, ili sitwae tena mali za watu?

Akamwambia, wewe umekwenda katika shamba la watu, mamayo ameniambia, ukaenda ukayachuma matango ya watu, wenyewe wakaja wakushtaki nyumbani, mamako amekunyang'anya tango, amewapa mwenyewe.

Baba yangu, sina la kunena, kinwa kimejaa maji, na nikinena nakuogopa, baba yangu, kuona hasira nyingi, ukagomba na mkeo, kwa hayo anitendayo.

Ee mwanangu, unieleze, wala sina hasira, wala simwambii mke wangu, nataka niyajue mimi na roho yangu. Akamwambia, waniona baba ninapokonda. Akamwambia, nakuona, mwanangu. Akamwambia, mimi sipewi wali, ila ukoko, tena ukoko ulioungua, na kunena sithubutu, na mwanawe humpa kulia wali mwema, akampa na mwingine, akamfichia, ussubui ukitoka ukaenda kazini kumwita mwanawe chumbani, akampa ule wali uliomwekewa wa jana, akala pekeyake, na mimi najua sipewi, na kuambia babangu naogopa, kwani ninyi wazee mmenena, hawa waanawake uchungu watoto wao u katika nyonga, na ninyi waanaume mmenena, mtoto mwanamke kwa mamaye mwanamke, nawe, babangu, umeoa huyu mwanamke, anitunze, na mimi mwanao ntaweza mimi kijana kizima mwanamke nikija nikikwambia, baba nna njaa? Nije nikwambie, baba nataka mtama? Mimi mwana mwanamke shuti niende kwa yule mama yangu, nenda hataki nikija