Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/478

From Wikisource
This page has been proofread.
458
MASHAIRI YA LIONGO.


Naapa kwa Anjili na Zaburi ili kiapo,
Simke ngeufu pindi shari liwagazapo,
Naye keeza moyo katokoza shari lilipo.

Mtetea cheo mwenyi cheo ateteapo; hambiwi ni nawi hatta roho nengakoma.


Naitenda mja kwa wenzangu kapata sono,
Wala sina yambo siwatayi kwa mavongono,
Bali sikubali lenyi thila na matukano.

Ni mwofu wa ta nishikapo na oa mno; ni mui wa kondo sikiapo mbi kalima.


Siwagazi kondo msi lango kapiga kifa,
Hi kusifua kwambazo ni tule swifa,
Nitangamizapo kondo nzito tenda hakhafa.

Ni mwana shajighi mpendeza nyemi za kufa; kwa kucha mpeo na adui wa kunisema.


Bonapo harubu kiugua nawa na afya,
Kawana furaha ja arusi ya mzofafa,
Naikeza moyo kwa Muungu nisikhilafa.

Ni mwana asadi mpendeza nyemi za kufa; kwa kucha mpeo na adui kumbuya nyuma.




Nappa kwa Anjili na Zaburi ni viapo thabiti,
Simpi mgongo pindi ubaya ukinikabili,
Naye hukabilisha moyo haitafuta ubaya papo pote.

Agombeaye daraja mwenyi daraja zamani agombeapo uovu na uovu hatta roho nengafikilia ajali.


Najifanyiza mtumwa kwa watu kama mimi nipate heshima,
Wala sina jambo nao siwataji kwa kuamba,
Lakini sikubali lenyi unyonge na matukano.

Huyeyuka kama nta nishikwapo huyeyuka mno, ni muovu wa vita pindi nikisikia mabaya maneno.