mimi nalitaka mali, yee akataka rathi. Akamwachia chungu na kinu, hatta chakula kidogo hakumwachia.
Wale jirani zake huja wakaazima kinu, wakatwangia, wakiisha, wakampa mchele kidogo, akapika, akala. Na wangine huja, wakaazima vyungu, wakapikia, wakiisha, wakampa naye chakula kidogo. Killa siku kazi yake ni hii.
Akatafutatafuta nyumbani mwa babaye na mamaye, asipate kitu, ela mbegu ya maboga. Akatwaa, akaenda, akapanda chini ya kisima. Ukaota mboga, ukazaa maboga mengi.
Yule nduguye hana habari, akauliza watu—chakula anapata wapi ndugu yangu? Wakamwambia, kuazima watu kinu, wakatwangia, wakampa naye chakula kidogo, na vyungu vyake kuazima watu, wakapikia, wakampa naye chakula.
Ndugu yake akaondoka, akaenda, akamnyang'anya kinu na vyungu. Amekwisha, akaamka subui akatafuta chakula hapati. Akakaahatta saa a tatu, akanena, nitakwenda kuangalia mboga wangu, umeota. Akaenda, akaona maboga mengi yamezaa. Akashukuru Muungu.
Akachuma maboga, akaenda, akauza, akapata chakula. Ikawa ndio kazi yake killa siku kuchuma, kaenda kuuza. Ikipata siku ya tatu, killa mtu, aliokula maboga yale akaona matamu mno. Killa mtu huchukua nafaka wakamwendea pale pahali pake, wakanunua. Siku nyingi zimepita, akafanya mali.
Mke wa ndugu yake akasikia habari ile, akatuma