Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/380

From Wikisource
This page has been proofread.
360
HASSIBU KARIM AD DINI.

Wakafuatana, wakaenda, hatta walipofika, Sultani wa nyoka akamwambia, sikukwambia, utakuja niua? Akamwambia, si mimi, na angalia maongoni mwangu. Akamwuliza, nani amekupiga hivi? Akamwambia, waziri. Akamwambia, bassi, sasa mimi nimekwisha kufa, lakini sharti unichukue wewe hatta kwenu. Akamchukua, na wale asikari wakarudi, na yule waziri yumo mlemle.

Akamwambia njiani rafiki yake, mimi nikifika nitauawa, na nyama yangu itapikwa, povu la kwanza, waziri atakwambia kunywa wewe, nawe usinywe, litie chupani, u'mwekee, la pili kunywa wewe, utakuwa tabibu mkubwa, la tatu ndio dawa la Sultani wenu. Na hili la kwanza akija akikuuliza, umekunywa wewe la kwanza? Mwambie, nimekunywa, na hili la pili lako weye. Waziri atapokea, akiisha kunywa, atakufa, utapumzika roho yako.

Wakaenda zao, hatta wakafika mjini, wakafanyiza vilevile kama alipomwagiza rafiki yake.

Yule waziri akanywa, akafa, na lile la pili akanywa yeye, na la tatu akamfanyia dawa la Sultani, akapona.

Akampenda sana Sultani, akawa tabibu mkubwa katika mji, akakaa raha kwa uzima hatta khatima.