Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/376

From Wikisource
This page has been proofread.
356
HASSIBU KARIM AD DINI.

mwambia, ninazo mimi. Akaniambia, nipe mwenyewe, nataka kuenda zangu. Nikamwambia, mimi nakupenda sana, nataka kukuoa. Nataka kwenda kwa baba yangu. Nikamwambia, huendi.

Wakaruka wale nduguze, wakaenda zao, nikamchukua kwetu, yule baba yangu akanioza. Akaniambia, nguo hizi usimpe, zifiche sana, akizipata mwenyewe, ataruka kwenda zake kwao. Nikazichimbia chini, nikazitia.

Hatta siku hiyo nimetoka kwenda kutembea, akazifukua, akazivaa mwenyewe akaruka, akakaa juu ya dari, akamwambia mtumwa wake, bwana wako akija mwambia nimekwenda zangu kwetu, kama anipenda anifuate. Akaruka, akaenda zake.

Hatta nilipokuja, nikaambiwa, mkewo amekwenda zake kwao. Nikapotea nikimfuata miaka mingi.

Hatta nilipofika karibu na mji nikaona watu, wakaniuliza, weye nani? Nikawaambia, mimi Jani Shah. Mtoto wa nani? Nikawaambia, mtoto wa Taighamusi. Wakaniambia, weye ndiye uliye umeoa bibi yetu? Nikawauliza, nani bibi yenu? Wakaniambia, Seyedati Shemsi. Nikawaambia, miye. Moyo wangu ukafurahi sana.

Wakanichukua hatta mjini kwao. Akamwambia babaye, huyu ndio mume wangu aliyenioa. Nikapendwa sana, nikakaa siku nyingi.

Babaye akaniambia, mchukua mkewo, kama wataka kwenda kwenu. Tukapewa Majini, wakatuchukua kwa siku tatu. Tukafika, tukakaa mwaka.

Nikasema, twende, tuangalie baba yetu. Mke wangu akaniambia, twende. Hatta tukifika hapa, mke wangu