Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/334

From Wikisource
This page has been proofread.
314
UZA GHALI.

akanena, na'am, inna kweli maneno haya. Akamwambia, nipe maana, waziri, ya mafungu manne haya.

Akamwambia, la kwanza, Sultani, lilitoswa baharini fungu moja, na moja lalipigwa moto, na moja lalikopeshwa wala hatalipwa, na moja amelipa wala hajaisha kulipa.

Akamwambia, na'am waziri, inna maneno yako kweli. Akamwambia, nipe maana ya kutoswa baharini fungu moja hili.

Akamwambia, ni mali aliotwaa Ali akaenda kufanya uasherati nje, mali yale yakapotea, ndiyo maana ya kuambiwa, fungu moja lile limeingia baharini.

Akamwambia, na'am waziri, inna neno hili kweli. Sultani akanena, hii fetha kwisha kupeleka waanawake fetha haipatikani tena, kweli maneno yake, kama imeingia baharini. Nipe na maana ya fungu la pili liliopigwa moto, nipe maana yake.

Akanena waziri, Ali alikula sana, alivaa sana, alitumia sana, ndiyo maana ya kupigwa moto mali zile, hazitaregea tena mkononi mwake.

Sultani akanena, na'am inna kweli maneno haya, waziri, kwani hii mali ukiisha kununua chakula, ukanunua na nguo njema, ukavaa, imekwisha potea mali hairudi. Maneno yake amenena kweli Ali, kama fungu hili limepigwa moto. Akamwambia, nambie, waziri, katika fungu la tatu maana yake.

Waziri akanena, fungu la tatu amelikopesha, wala hatalipwa. Akamwambia, maana yake nini ya kukopesha mali hayo wala hatalipwa? Waziri akanena, ni mali aliyetoa kumpelekea mahari yake manamke, utapomwacha,