Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/322

From Wikisource
This page has been proofread.
302
UZA GHALI.

Akamwambia—Ee Walla! Ee Walla! namjua anakokaa. Kule-e-e mwisho wa mji, kuna kipenu kidogo karibu na pwani, ndiko anakokaa kwa yule masikini mwenyi chongo anayopita akiomba, ndiye rafiki yake, ndiko anakokaa, hana pahali pangine.

Akaondoka waziri usiku, saa ya sita, watu pia wamelala, yeye na mtumwa wake mmoja, huyu mtumwa ndiye msiri wake, wakaenenda hatta wakafika. Akabisha yule waziri katika kile kipenu, akamwita—Ali! Ali! Akaogopa, asiitike. Akamwambia—Ali!

Akamwambia rafiki yake, amka, amka. Akamwuliza, kuna nini? Akamwambia, kumepiga mtu kibandani kwetu, nami nataajabu usiku huu, huyu mtu mlevi, ao mtu atakayokuja kwiba huku ndani? Lakini sisi fukara, hatuna kitu. Labuda mtu ataka kutuhusudu, kututoa roho zetu. Akamwambia, lakini mimi, na tukae kitako kwanza tusikilize, hatta atakapobisha mwango huu marra ya tatu tumwitikie, hwenda tukamjua sauti yake.

Akamwambia, gissi gani wewe, Ali, kuwa mjinga? Mtu amekuja usiku wa manane, hatumjui atokako, na sisi hatuna kawaida ya kuja mtu kubisha mwango kwetu, ataka nini mtu huyu, isipokuwa labuda ana mambo matatu ataka kwetu, kama Muungu amenijalia mambo haya nayawaza mimi katika roho yangu, ni lile apendalo Mwenyi ezi Muungu.

Akamwambia Ali—Gissi gani, rafiki yangu, maana ya tatu gani haya, unayowaza wewe katika roho yako? Nambie nami najue, tupate kujua sote. Nambia la kwanza.

Akamwambia, la kwanza, ataka kuja kwiba; la pili, ataka kuja kutuua; la tatu, labuda anasema huku kuna mke wake, ao mtumwa wake mwanamke. Ndiyo ninayoyawaza