Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/320

From Wikisource
This page has been proofread.
300
UZA GHALI.

Akaondoka waziri wake Sultani palepale, katika baraza, akamwambia—Seyedina, maneno haya nayajua maana yake. Sultani akamjibu, akamwambia, kamma wee uyajuapo maneno haya maana zake, billa kumwuliza Ali, uyajue kwa akili yako, mimi Sultani ntakupa usultani wangu, kinachosema na kisichosema katika milki yangu, mimi Sultani nimekupa, yako. Na wewe usipojua maneno haya maana zake kwa akili yako, mali yako nitatwaa yote, wallakini usimwulize Ali.

Akanena waziri, nisipojua maneno haya kwa akili zangu, mimi waziri katika milki yangu nimekupa, Sultani, kinenacho na kisichonena, illa mke wangu mtoto wa watu enda kwao, na kitwa changu halali yako, Sultani.

Sultani akanena, na mimi ntashuka katika ufaume niwe ndiye waziri wako, mimi Sultani.

Akaondoka waziri, akaenda hatta nyumba yake, akanama, akafikiri, akaenda akatwaa vyuo viliomo jamii ndani ya nyumba yake. Akavifunua kutazama maana ya maneno ya Ali, asipate kimoja kilichomo maneno ya Ali. Bassi akakaa kitako akifikiri na kuaza—mimi nimenena kwa Sultani, maneno haya ntayajua kwa akili zangu, nami nimetafakari na kuwaza sikuyajua.

Akamwita, Juma! yule kijana Ali anakaa wapi? Akamwambia, Bwana, Ali gani?

Akamwambia, kile kijana aliokuwa na mali mengi, kijana cha waziri marehemu Hassan, aliofilisika humjui anakokaa? Tafáthali unipeleke, nna maneno naye kutaka kumwuliza. Na maneno haya nimekwambia wewe, usimwambie mtu tena. Nami nimekuacha huru kwa sababu maneno haya asijue mtu.