Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/308

From Wikisource
This page has been proofread.
288
MWALIMU GOSO.

ikaangusha buyu, likampiga mwalimu wetu Goso, si mtende. Kiyambaza kikanena, kwamba mimi ni bora, ningalizuliwa ni panya?

Wakaenenda wakanitwaa panya, wakampiga. Yule panya akanena, mwanipiga, nimefanya nini? Wakamwambia, wewe panya mzua kiyambaza, na kiyambaza mzuia kusi, na kusi ikaangusha buyu, likampiga mwalimu wetu Goso, si mtende. Yule panya akanena, kwamba mimi ni bora, ningaliliwa ni paka?

Wakaenenda wakamtafuta paka, wakamtwaa, wakampiga. Yule paka akanena, mimi mwanipiga, nimefanya nini? Wakamwambia, wewe paka mla panya, na panya mzua kiyambaza, na kiyambaza mzuia kusi, na kusi ikaangusha buyu, likampiga mwalimu wetu Goso, si mtende. Yule paka akanena, kwamba mimi ni bora, ningalifungwa ni kamba?

Wakaenenda, wakaitwaa kamba, wakaipiga. Ile kamba ikanena, mimi kamba mwanipiga, nimefanya nini? Wakamwambia, wewe kamba mfunga paka, na paka mla panya, na panya mzua kiyambaza, na kiyambaza mzuia kusi, na kusi ikaangusha buyu, likampiga mwalimu wetu Goso, si mtende. Ile kamba ikanena, kwamba mimi bora, ningalikatwa ni kisu?

Wakaenenda, wakatwaa kisu, wakakipiga. Kile kisu kikanena, mimi mwanipiga, nimefanya nini? Wakamwambia, wewe kisu mkata kamba, na kamba mfunga paka, na paka mla panya, na panya mzua kiyambaza, na kiyambaza mzuia kusi, na kusi ikaangusha buyu, likampiga