Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/292

From Wikisource
This page has been proofread.
272
SULTANI MAJINUNI.

Akawaambia, leo roho yangu naiona itapata mambo matatu katika ulimwengu kwa siku ya leo. Wakamwuliza, la kwanza, bwana? Akawaambia, la kwanza, leo naona roho yangu, ntakufa. La pili, bwana? Nathani leo nitampiga nunda. La tatu, bwana? Akanena, nathani ntaonana na mama yangu, ntaonana na baba yangu ntaonana na mjumba wangu, ntaonana na shangazi langu, ntaonana na ndugu zangu, ntaonana na wote rafiki zangu. Wakamwambia, heri, bwana.

Wakakaa kitako pale, wakapakua wali, wakala, wakala sana, wakashiba. Wakaondoka. Akawaambia, na tupande sasa juu ya mlima. Wakamwambia, Ee walla, bwana. Akatangulia na watumwa wake, Shindano na Kiroboto. Wakapanda, wakaenda hatta walipotupa macho nuss ya mlima, wakaona chini mbali sana, wakaona na juu mbali. Akawaambia, msiogope na twende. Wamwambia, na twende hatta tufike juu ya mlima, tusipande juu ya kilele.

Wakaenda hatta walipofika juu ya mlima macho yao yaona mbali. Akawaambia, na tupumzike hapa juu. Hapa nafasi tele. Bassi wa leo tulale kuku huku hatta kesho, tufanye shauri. Wakamwambia, vema, bwana.

Akaondoka yule mtumwa wake mmoja, akazungukazunguka juu ya mlima. Alipotupa macho chini, aona nyama mkubwa, lakini kule chini kiza kwa miti hamwoni vema. Akamwita, Bwana! Bwana! Akamwitika, naam. Akamwambia, njoo tazame, bwana. Akaenda hatta akifika pale aliposimama Shindano, akamwambia, tupe macho