khofu ya nini mama? Akamwambia, kama khofu yako mama ya kufa, nitakaa hatta lini, sina buddi ntakufa. Akamwambia, naenda zangu. Akamwambia, kua heri.
Akaenda akaingia katika msitu na nyika, akaenda, akamkamata twiga. Aka'mua, akafurahi sana roho yake, akanena, huyu ndio khalisi nunda. Akamfunga, akamkokota, hatta akija akikoma nuss ya njia, akaimba,
Mama wee, niulaga
Nunda mla watu. (Marra kenda.)
Mwanangu, si yeye
Nunda mla watu. (Marra tano.)
Akatwaa akamwacha.
Akamwambia, mwanangu, taabu unazo kupata peke yako, nawe unao nduguzo watu watatu hapa, hapana mmoja anaonena, naswi tumfuate yule mdogo wetu, kwenda naye mwituni, tukamtafute huyu nunda. Hapana. Wote wamekaa kitako na shughuli zao, unasumbuka peke yako, mwanangu. Akamwambia, tumbo waliotoka wewe ndio waliotoka wale, na baba yenu ndiye mmoja Sultani Majnuni. Si kwamba mna baba wawili, ukasumbuka peke yako, lakini baba yenu ndiye huyu mmoja. Akamwambia, mama killa mtu ana roho yake, tungezaliwa tumbo moja, na killa mtu ana roho yake. Akamwambia, bassi mwanangu usiende, hizi siku walizokwenda bass. Akamwambia, mama ndilo jambo lisio buddi, sina buddi ntakwenda. Mamaye akalia sana, na babaye akalia sana, sababu wamefanya khofu, kwa mwanetu atakufa, na huyu ndio mwana bora tulionaye. Lakini tutafanyaje? Hakubali kukaa.
Akaenda msitu na nyika, hatta akaenda akamkuta faru,