itakapokuwa katika bahari, ntakuja. Akamwambia, vema. Akaruka, akaenda zake.
Mtoto akirudi katika mtende, akauona mtende, akaziona na tende, akaona na roho yake imefurahi, moyo uliona nafsi yake kama alikuja mtu akamwambia, haya ondoke ende peponi, gissi ya roho yake alivyoiona nzuri, alivyoiona imefurahi, alivyoiona mwili wake na nguvu, anavyojiona macho yake yana nuru. Akacheka kijana sana, akanena hii ni bahati yangu mimi, mkaa jichoni. Walikuja simba sita hapa, killa mtu upanga na ngao, na jamvia kiunoni, na bakora mkononi, na killa kijana amwambia mwenziwe, jongea huku nipishe nami. Kwanza vijana vina nguvu, la pili vijana vizuri, la tatu wajuikana sana katika mji kuliko mimi mkaa jichoni. Lakini hii bahati yangu Muungu amenipa. Kiwekwacho na Muungu, mwana Adamu hawezi kukiondoa, illa yeye aliokiweka.
Akiondoka kijana akamwambia, mtende, kua heri, nami nakwenda lala, alio akikula, sasa hatakula tena, leo hili limekuwa zingizi kumkomesha mzazi. Akaondoka, akaenda akalala.
Hatta usiku ulipopambauka, akija hatta pale mtendeni akajifunuka shuka, akalala. Hatta nokoa wake akaamka. Nikautazame mtende huo leo, kama tutapata haya makombo ya ndege yanaosalia, kwani mtende huu, mtu hauoni tende. Akija nokoa, hatta alipokoma nussu ya njia alipotupa macho kunako mtende kule, akauona mtende umemkalia tamu.
Akirudi mbio hatta nyumbani akipiga goma, wote wajoli wake wakaja, wake kwa waume, hatta watoto