Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/252

From Wikisource
This page has been proofread.
232
SULTANI MAJINUNI.

ni changa, hasadiki. Na killa tawi lamwambia mwenziwe, jongea huku, nipishe mimi nikae.

Akamwambia, nasikitika mimi mtu mwenyi watoto saba, miaka mitano mtende wangu umeliwa na ndege, sikupata kulimbuka hatta kokwa moja, na mwaka huu vilevile, utaliwa na ndege.

Yule mtoto aliokaa jikoni akasikia maneno yale aliyoyanena Sultani Majnuni. Akaondoka yule kijana, akamwambia, baba, mwaka huu utakula tende. Akamwambia, baba yangu, kama mwaka huu sikukulisha tende kwa mkono wangu, na jamii ya matajiri yaliomo katika mji, na jamii ya Wazungu waliomo katika mji, na jamii ya Banyani waliomo, na jamii ya Wahindi waliomo, na maskini waliomo katika mji wetu, kwani haya ni matawi matano yaliomo katika mtende. Akamwambia, bassi, killa tawi ntawapa kabila mojamoja, na kabila ziliomo katika mji ni tano, mna sisi Waarabu, mna na Wazungu, mna na Banyani, mna na Wahindi, mna na jamii za maskini waliomo. Akamwambia, bassi mimi baba ninakwenda mwaka huu, kwenda kuungoja mtende.

Baba yake na mama yake wakacheka sana, wakaona maneno yake yale yote upuuzi. Babaye hakukubali maneno yale, wala mamaye, wanamwona, mwanetu anazumgumza, na tumwache azumgumze hatta shauko yake yamwishe ya kuzumgumza.

Hatta akaletewa khabari Sultani, tende zimewiva. Akatoa khabari Sultani ya kutafuta mtu kwenda kuungojea mtende. Yule mwanawe aliobaki wa saba akasikia, akamwambia, ginsi gani, baba, umetoa khabari ya kutafuta mtu wa kuungojea mtende, nami mwanao mmoja nipo bado nimesalia. Akamwambia, Ah! sita hawakufaa,