Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/250

From Wikisource
This page has been proofread.
230
SULTANI MAJINUNI.

zimeliwa na ndege, hatukupata hatta moja, nasi tumekuja, wewe kisu, sisi nyama, utakalo lote, ututende? Akamwambia, vema, twende zetu.

Wakaenda hatta kwa baba yao. Wakamkuta, amekaa ukumbi wa ndani. Wakamwamkia, asiitikie. Akaondoka mkewe akamwambia, Bwana, watoto wakikuamkia, waitikie, kwani hasira yako ndio sumu yao ya kuwaua, na furaha yako ndio uzuri wa uso wao; bassi ufanyapo hivyo wewe, uwakasirikia watoto wako wambao uwaweza kuwatenda killa jawabu. Bassi huna haja kuwakasiri, wala kuwafanyia ghathabu, wala usiwafanye uchungu. Bassi, mke wangu, kawakatie kisuto, na kisuto wape na ukaya, kwani vijana hivi vimekuwa waanawake, hawamfai mtu ulimwenguni ali mzima, watamfaa mtu akhera? Lakini miye bassi, sina shughuli nao.

Wakakaa hatta muda wa miezi kupita, mtende ukazaa, ukawacha kuzaa, ukawayawaya. Mwenyi kuziona tende ndogo, nazo changa, mtu akiziona mbali hunena pevu, kwa ginsi ya tende kuwa nene, kwa ginsi ya mtende kusitawi, na tende gissi ya kuwa na nguvu, na killa tawi limejaa sana.

Akaondoka nokoa kwa mguu wake hatta kwa bwana wake, akamkuta bibi yake. Akamwambia, Bibi, bwana yu wapi? Akamwambia, yuko ndani, ngoje. Asipate mda akatoka kule ndani, akamwambia, Je! Nokoa! khabari ya shamba? Akamwambia, Shamba, bwana, kuzuri, shamba kwema, na khabari za shamba bwana, mtende umekithiri kuzaa, tena zimekuwa nene tende, ukiziona hapo zilipo changa, mtu hunena pevu, na akiambiwa hizi