Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/202

From Wikisource
This page has been proofread.
182
MOHAMMADI MTEPETEVU.

Wakanichukua, wakaenda nami hatta kwa mfalme wao. Yule mfalme wao ajua kusema Kiarabu na inchi yenyewe katika inchi za Kihindi.

Bassi yule mfalme akasema nami kwa lugha ya Kiarabu, akaniuliza khabari zangu, nitokako, nilivyokwenda, hatta nikaokotwa katika bahari. Bassi nikampa khabari zangu zilionipata. Yule mfalme akamwita waziri wakwe, akanitwaa mimi, akampa waziri wakwe, akamwambia, u'mweke kwako, ukamtenda vema hatta arudi hali. Bassi nikaenenda nikamfuata. Akaenenda akanipa nyumba njema, malalo mema, makula mema, kwa killa jambo la wema akanitenda.

Nikakaa siku nilizokaa kwake. Na katika nyumba ile naliokaa ina bustani, nikakaa siku hiyo nikafungua dirisha ile iliolekea bustani, nikatezama, ikanipendeza mno bustani ile. Nikaona mto wa maji ndani yake, nikapenda kwenda kuoga katika mto ule. Nikashuka, nikaenda nikaingia ndani ya maji, nikaoga. Bassi nikaufuata mto ule, ukanitoa mji.

Nikitahamaka, sikujua nitokako, wala nendako, nikawa kama mtu wa kupigwa na bumbuazi. Bassi marra ile, nikamwona mtu amepanda frasi, akanijongelea hatta nilipo. Akaniita kwa jina langu. Akaniambia, jamala yako haipotei. Akaniuliza, wanijua mimi? Nikamwambia, sikujui. Akaniambia, yule nyoka mweupe ndimi nduguye. Na sasa nimekuja kulikhatimisha jambo letu. Akaniita, akaniambia, njoo, tupande frasi, tukapanda wawili frasi, tukaenenda.

Akaniambia, sasa tumekaribia mji wa Nuhás. Nami sijui nitokako, wala sijui nendako. Sijui mbele, sijui nyuma, nimekuwa mtu tu. Tukaenda, tukafika pahali pana