Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/186

From Wikisource
This page has been proofread.
166
MOHAMMADI MTEPETEVU.

nyama zao. Akasalia Sheikh Abalmathfár na jamaa zake watu wawili, na nuss ya baharia. Wakafungwa, ili kuchinjwa assubui.

Hatta ilipofika usiku akaondoka yule kima, akafungua yeye kwanza, akaisha akafungua Sheikh Abalmathfár, akaisha akafungua na wale jamaa waliosalia, hatta akawaisha pia yote. Sheikh alipoona wamefunguliwa, wakakimbia wakaenda zao merikebuni kwao wakaiona bado mzima, haijavunjika, wakatweka, wakakimbia. Wakaenda katika bahari kule katika kuja zao.

Na watu katika merikebu mle huzamia lulu. Alipoona kima yule watu wanazimia lulu, naye akajitosa pamoja nao. Sheikh akasema, nimekwisha potea kwa bakhti ya yule maskini ya Muungu. Hatta zamani waliporejea watu, naye akarejea nao. Amechukua na lulu, na lulu zake njema kuliko za watu. Akamtupia bwana wake miguuni pake.

Bassi akawaambia jamaa wale, kama sisi hatungepona ela kwa sababu ya kima huyu, bassi killa mtu na atoe dinari thenashara mia, tumpelekee bwana wake, killa mtu dia ya roho yake. Wakatoa, akazikusanya Sheikh Abalmathfár, akatanganya na lulu zile alizopata kima. Na fayida ya dirhamu tano zangu akatia ndani ya makasha akafunga, akaandika alama ya Mohammadi mtepetevu.

Bassi wakasafiri hatta wakafika inchi ya Bássara, wakapiga mizinga, wakashuka.

Mama yangu akasikia kama Sheikh Abalmathfár amekuja, akaja akaniambia, toka wenende ukamtazame Sheikh Abalmathfár, ukampe mkono wa salama. Nikamwambia, siwezi kwenda, njoo niondoe. Akaniondoa, aka-