Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/184

From Wikisource
This page has been proofread.
164
MOHAMMADI MTEPETEVU.

Nami nikajirudia nyumbani kwangu, ikawa hali yangu ile ile, kulala na kulishwa, na kunyweshwa maji.

Sheikh akasafiri yule, akaenda zake katika inchi ya Sini. Wakafanya biashara zao hatta wakaisha. Wakasafiri, wakaenda mwendo wa siku mbili, dirhamu zangu zile akazisahao, asininunulie kitu. Akazikumbuka baada ya siku mbili. Akawaambia matajiri wenziwe, kama hatuna buddi na kurudi, amana ya Mohammadi mtepetevu nimeisahao. Wakamjibu matajiri wenziwe, wakamwambia, utarudi kwa sababu ya dirhamu tano, naswi tumepakia mali mengi ndani ya merikebu? Akawaambia kana hamtaki kurudi mkamfanyizie killa mtu kitu maalum. Wakakubali wale matajiri.

Bassi wakaja safiria wakaenda hatta wakawasili katika kisiwa. Na kisiwa kile kimekwitwa, kisiwa cha Sunudi, ndio jina lake. Wakashuka pale, ili kwenda kupumzika kwa taabu ya bahari ile. Wakatembea mjini mle.

Yule Sheikh niliyempa amana yangu, akapita mahali dukani, akaona kima wamefungwa, pana na mmoja mdogo wao amenyonyoka manyoya pia, na wale wenziwe humpiga. Bassi Sheikh alipomwona, akamwonea huruma, akamtaka kwa mwenyewe, akamnunulia kwa dirhamu zangu tano. Naye Sheikh nia yake kuniletea kuchezea, kwani amenijua ni mtu sina kazi.

Wakasafiri wakaja zao hatta kisiwa cha pili. Kisiwa kile kinakwitwa kisiwa cha Sodani, kwani wenyewe na watu wenzi wao hula nyama za waana Adamu. Walipoona merikebu imefika pale, wakaipandia wakaenda wakawafunga watu waliomo pia wote, wangine wakachinja, wakala