Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/122

From Wikisource
This page has been proofread.
102
SULTANI DARAI.

frasi mimi naye tukatembea, wala hatujapata kutanganya mimi naye tukala, na kuondoka naona hasara. Akamwambia, Bwana huna buddi kwani yeye anataka upesi kwenda kwao, baada yeye ameniambia, kama yeye amekaa siku nyingi. Akamwambia, Vema. Akaenda zake, akamjibu bwana wake. Akamwambia, nimemwambia mkwewo mashauri yako, amerithika. Akamwambia, Bassi amruni waambie jamii ya watu, kama muda ya siku nne Sultani mwanawe anakwenda kwa mumewe, nanyi 'mwe na habari.

Sultani akawaambia watu walio katika mji, wake kwa waume, siku ya kwenda mwanangu, na waanawake wa kiungwana wamfuate. Akatoa na watu, akawaambia, ninyi kaeni mkimtazama mwanangu katika njia.

Hatta muda ilipokoma siku ya nne wakatoka wangwana wote waanawake walio bora, na watumwa wao, na frasi zao, wakaingia katika kundi kumpeleka mwana wa Sultani kwa mumewe, Sultani Darai. Wakatokea, wakaingia katika njia, wakaenda hatta lilipokoma jua vitwani, wakapumzika. Paa akaamru kufanyiza vyakula vema, wakala tokea wangwana hatta watumwa, wakashiba sana na roho zao zikafurahi kwa zakula kuwa zema.

Wakaenda hatta ilipokoma saa kumi na moja. Akawaambia, wangwana hapa na tukae, mahali pa kulala. Vikafanyizwa vyakula vema na wali mzuri, wakala wangwana hatta watumwa. Wakafurahi wangwana hatta watumwa wakalala pahali pale. Bassi usiku alianza tokea pembe hatta pembe, tokea mwanzo hatta mwisho, kwa wangwana na watumwa, hatta kwa nyama zalizopandwa, pasiwe mtu mmoja alioikosa heshima yake, tokea watumwa hatta wangwana, hatta nyama zao walizopanda, na wote walifurahi kwani yeye apenda sana kumfurahisha bwana wake. Akamwita, Baba! akamwambia, naona umechoka