Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/112

From Wikisource
This page has been proofread.
92
SULTANI DARAI.

panga na ngao. Akamwambia, mama, hayo yamepita, tazama na yangu. Akamwambia, baba, kuwa hawakuwa wenyi miguu miwili, utakuja kuwa wewe, mwenyi miguu minne. Akamwambia, mama, masifiwa sikuona sifa, nda kujionea.

Akamwambia, napenda mtoto, urudi ulikotoka. Akamwambia, si jambo la kupatikana, mama, pale, nalikokwambia niregee nyuma tena. Walinambia nini kwanza? Akamwambia, sikuambia, nzi kufia tuini si hasara? Akamwambia, kweli umeniambia, nami, mwanangu, simekujibu? Akamwambia, walinijibu nini mama? Akamwambia, sikukwambia, nakuonea hasara? Akamwambia, hasara yako mbona sipendelei sana. Akamwambia, mimi sina buddi kukuuliza pindi usiniambie, lakini ntakuuliza, mwenyi nyumba hii nani?

Akamwambia, Oh!—baba wee, nyumba hii ina wingi wa mali, ina wingi wa watu waliomo, ina na wingi wa zakula ziliomo, ina na wingi wa frasi waliomo, bassi na mwenyewe mji huu wote ni nyoka mkuu mno wa ajabu.

Ehée! mzee, nipe busara nipate nyoka huyu, hatta nimpate nimwue. Akamwambia, Oh! mwanangu, maneno haya usinene, utanichongea, tena kuko aliko yeye mwenyewe alisikia tena, nimewekwa mimi pekeyangu hapa, mimi mzee, kazi yangu ya kupika zakula; wayaona masufuria yale, bassi anapokuja yule joka hapa, kuvuma baridi na vumbi kuruka kama methili ya tufani inapokuja. Bassi akija, hufikia pale uwanjani, akala hatta akashiba, akaingia hapa ndani kunywa maji. Akiisha kunywa maji,